LENGO LA MRADILengo la mradi ni kusaidia kuleta maridhiano ya kisiasa baada ya uchaguzi kupitia midahalo na majadiliano ya wananchi na wadau wadau wote hasa wanasiasa, viongozi wa dini na asasi za kiraia ili kuleta amani ya nchi baada ya uchaguzi hivyo mradi umelenga Kuhimiza midahalo, majadiliano ya amani na mashirikiano baina ya wadau na Kuongeza mwamko na kuleta tija katika jamii juu ya juhudi za kuzuia migogoro na usuluhishi kwa njia ya amani. Ili kufikia lengo, shirika la SFCG inazialika Asasi za Kiraia na Jumuiya za Zanzibar zilizosajiliwa, zenye uwezo na ujuzi wa kufanya miradi kwenye eneo la ujenzi wa amani na kuleta maridhiano ya kisiasa Unguja na Pemba kuomba ufadhili wa shughuli watazozibuni wenyewe kulingana na mazingira yao ili kuchangia juhudi za kuleta amani na maridhianoLENGO LA MRADILengo la mradi ni kusaidia kuleta maridhiano ya kisiasa baada ya uchaguzi kupitia midahalo na majadiliano ya wananchi na wadau wadau wote hasa wanasiasa, viongozi wa dini na asasi za kiraia ili kuleta amani ya nchi baada ya uchaguzi hivyo mradi umelenga Kuhimiza midahalo, majadiliano ya amani na mashirikiano baina ya wadau na Kuongeza mwamko na kuleta tija katika jamii juu ya juhudi za kuzuia migogoro na usuluhishi kwa njia ya amani. Ili kufikia lengo, shirika la SFCG inazialika Asasi za Kiraia na Jumuiya za Zanzibar zilizosajiliwa, zenye uwezo na ujuzi wa kufanya miradi kwenye eneo la ujenzi wa amani na kuleta maridhiano ya kisiasa Unguja na Pemba kuomba ufadhili wa shughuli watazozibuni wenyewe kulingana na mazingira yao ili kuchangia juhudi za kuleta amani na maridhiano.SHUGHULI LENGWA KATIKA UTEKELEZAJI;

SFCG inalenga kufadhili shughuli mahsusi shughuli zenye sifa zinazotajwa hapa chini;

    • Shughuli zinazotarajia kukuza uelewa wa jamii juu ya utambuzi na utatuzi wa vyanzo vya mgogoro na ushiriki wa jamii katika utatuzi wa migogoro yao.
    • Shughuli zinazolenga kuimarisha ushiriki wa vijana na wanawake katika mijadala ya amani.
    • Shughuli zinazotarajia kuchangia kukuza mashirikiano, utangamano baina ya makundi mbalimbali katika jamii husika ili kuondoa migogoro ya kisiasa, kuleta maridhiano na kudumisha amani.
    • Shughuli zinazolenga kutatua migogoro ya kisiasa kwa wanajamii moja kwa moja kwa kushirikisha wadau mbalimbali.

      KIWANGO CHA UFADHILI NA UTARATIBU WA SHUGHULI ZITAZOPENDEKEZWA

        • Gharama za shughuli za mradi hazitatakiwa kuzidi Tsh 2,000,000/= SFCG itasimamia masuala yote ya fedha (italipia mojamoja huduma na malipo) ili kuwezesha shirika kutumia ujuzi wao kutekeleza shughuli zitazopendekezwa. Ikiwa mradi utahusu manunuzi ya chakula, steshenari au ukodishaji wa kumbi za mikutano basi zitatumika taasisi au biashara zilezile zilizoingia mkataba rasmi na shirika la SEARCH FOR COMMON GROUND ili kuleta ufanisi na shughuli zifanyike kwa wakati.

          VIGEZO VITAKAVYOZINGATIWA KATIKA KUIDHINISHA MIRADI

            • Kigezo kikuu kitakachozingatiwa katika kupata ufadhili huu wa shughuli ni kwamba shughuli za mpango husika zitathibitishwa kuwa zinachangia katika kuleta Amani na maridhiano hapa Zanzibar.

              Vigezo vingine mahsusi ambavyo vitazingatiwa katika uidhinishaji wa mradi ni;

                • Ni kwa jinsi gani shughuli husika, itachangia matokeo chanya ya kuleta Amani na maridhiano ya kisiasa hapa Zanzibar.
                • Ubunifu wa shughuli ya mradi yenye kuleta tija kwa gharama isiyozidi milioni mbili.
                • Nafasi ya jamii na ushirikishwaji - kiwango cha uhusishwaji wa jamii hususan kutoka ngazi za chini kabisa na makundi maalum hasa Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
                • Utekelezaji wa shughuli hizi hautachagua mashirika bali wazo bunifu, utayari wa shirika katika kutekeleza ndani ya wakati husika.
                • Jinsi na namna ambavyo shughuli husika itahusisha Taasisi na Mamlaka husika za Serikali katika utekelezaji ili kuleta uendelevu wa mradi.

                  TAASISI NA SHUGHULI ZISIZOLENGWA KUPATA RUZUKU.

                    • Taasisi ambazo zimesajiliwa, kufanya shughuli zake kwa mujibu wa Sheria na ambazo hazizalishi faida. (Jumuiya)
                    • Vikundi rasmi vya vijana, wanawake na makundi maalum vilivyosajiliwa na visivyozalisha faidaKama maelezo na ufafanuzi zaidi vitahitajika juu ya kigezo hiki, basi wasiliana na SFCG kabla ya kufanya maombi ya uwezeshwaji.

                      UFADHILI WA SHUGHULI HAUTALENGA SHUGHULI ZIFUATAZO;

                        • Shughuli zitazofanyika nje ya Zanzibar
                        • Shughuli ambazo tayari zimeshawahi kufanyika na kukamilikaUfadhili wa shughuli zenye mwelekeo wa kuibua migogoro baina ya makundi ya kijamii
                        • Shughuli zinazolenga kunufaisha dini, dhehebu au kabila au kikundi chenyemlengo wa kikabila FulaniShughuli zenye nia ya kutunisha mfuko wa asasi au mtu binafsi
                        • Shughuli ambayo imekwisha wezeshwa na mashirika mengine.
                        • Shughuli ambazo zinakiuka sheria, taratibu na mila

                          UTARATIBU WA UOMBAJI

                            • Vikundi visivyo rasmi, Mashirika, Jumuiya, ASASI na Taasisi zisizo za Serikali Zanzibar zinazokidhi vigezo wanaalikwa kuomba ufadhili kwa kufuata utaratibu ufuatao.
                            • Maombi yanaweza kutumwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza . Jaza fomu mahususi iliyoambatanishwa hapa pamoja na tangazo hili

                              MASUALA YA KUJAZA KATIKA ANDIKO LA MRADI

                                • JINA SHIRIKA/ASASI NA KAZI MNAZOFANYA -Toa maelezo mafupi ya asasi yenu yasizidi paragrafu mbili
                                • MRADI UNAOPENDEKEZWA (TITLE)-Jina la mradi kwa ufupi
                                • SHUGHULI ZA MRADI UNAOPENDEKEZWA- shughuli mnazopendekeza kufanya
                                • MUDA WA UTEKELEZAJI (TIME FRAME)-Muda na Tarehe ya utekelezaji (Iwe ndani ya mwezi Octoba, 2022)
                                • MATOKEO -Andika nini mnatarajia baada ya kufanya shughuli mlizopendekeza
                                • WALENGWA/WANUFAIKA (BENEFICIARIES)-Taja kwa ufupi walengwa na wanufaikaji wa mradi
                                • AINISHO LA BAJETI (BUDGET BREAKDOWN)-Ainisha gharama zote za mradi mtazotumia (Isizidi milioni 2 fedha za kitanzania)ANGALIZO: MAELEZO YOTE YA HAPO JUU YASIZIDI KURASA MBILI TU (ONLY 2 PAGES)Mwisho wa kutuma maombi haya ni Tarehe 7 Oktoba , 2022 saa 10:30 jioniWasilisha ombi lako kwa njia ya kielectroniki kupitia mfumo wetu wa “LEVER” Maombi yote yatakayotumwa kwa njia Barua pepe, EMS/Rejesta au kwa mkono hayatapokelewa wala kufanyiwa kazi. KWA TAARIFA ZAIDI;Kwa mawasilino ya kawaida na maulizo (Inquiries) tafadhali wasiliana nasi kwa kupiga simu kupitia nambari +255 773 800623 au 0715230680, au email achikira@sfcg.orgAs job descriptions cannot be exhaustive, the position holder may be required to undertake other duties that are broadly in line with the above key responsibilities. Only applicants invited for an interview will be contacted. No phone calls, please. Please see our website www.sfcg.org for full details of our work. All Search Employees must adhere to the values: Collaboration- Audacity - Tenacity - Empathy - Results. In accordance with these values, Search enforces compliance with the Code of Conduct and related policies on Anti Workplace Harassment, Protection from Exploitation and Abuse, Child Safeguarding, Conflict of Interest, and Anti-fraud. Search is committed to safeguarding the interests, rights, and well-being of children, youth, and vulnerable adults with whom it is in contact and to conducting its programs and operations in a manner that is safe for children, youth, and vulnerable adults. Search for Common Ground does not and shall not discriminate on the basis of race, color, religion (creed), gender, gender expression, age, national origin (ancestry), disability, marital status, sexual orientation, or military status, in any of its activities or operations. View our code of conduct here and our privacy policy here.Les descriptifs de pouvant ne pouvant être exhaustifs, le titulaire du poste pourra être amené à entreprendre d'autres tâches qui correspondent globalement aux responsabilités clés ci-dessus.Seuls les candidats invités à un entretien seront contactés. Pas d'appels téléphoniques s'il vous plaît. Veuillez consulter notre site Web www.sfcg.org pour tous les détails de notre mission.Tous les employés de Search doivent adhérer aux valeurs de Search : Collaboration- Audace - Ténacité - Empathie - Résultats. Conformément à ces valeurs, Search fait respecter le code de conduite et les politiques connexes sur la lutte contre le harcèlement au travail, la protection contre l'exploitation et les abus, la protection des enfants, les conflits d'intérêts et la lutte contre la fraude. Search s'engage à préserver les intérêts, les droits et le bien-être des enfants, des jeunes et des adultes vulnérables avec lesquels elle est en contact et à mener ses programmes et ses opérations d'une manière qui soit sûre pour les enfants, les jeunes et les adultes vulnérables.Search for Common Ground ne fait pas et ne doit pas faire de discrimination fondée sur la race, la couleur, la religion (croyance), le sexe, l'expression de genre, l'âge, l'origine nationale (ascendance), le handicap, l'état matrimonial, l'orientation sexuelle ou le statut militaire, dans aucune de ses activités ou opérations.Consultez notre code de conduite ici et notre politique de confidentialité ici.

This vacancy is archived.

Recommended for you